Kulingana na gazeti la Mwanaspoti, Yanga wako kwenye mchakato wa kumsajili Stephano Ki Aziz mshambuliaji wa Asec Mimosas raia wa Burkina Fasso
Ki Aziz amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii wiki hii hasa baada ya mchezo kati ya Asec Mimosas dhidi ya Simba ambao Asec walishinda mabao 3-0 kule Benin
Ki Aziz alifunga moja ya mabao ya Asec katika mchezo huo lakini pia alifunga bao la Asec katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam na Simba kushinda mabao 3-1
Wakiwa na dhamira ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa msimu ujao, Yanga imeanza kufanyia kazi mapendekezo ya kocha Nasreddine Nabi ambaye ndiye aliyependekeza usajili wa nyota huyo
Hesabu za Yanga kwa KI ambaye amefunga mabao matatu katika Kombe la Shirikisho zilianzia hapa nyumbani baada ya Nabi kuona makali yake na kuwaagiza viongozi wamfuatilie
Habari njema ni kuwa maneja anayemsimamia Yacouba Songne ndiye Meneja wa Ki Aziz na tayari amemuunganisha na matajiri wa Yanga, GSM
"Tunaendelea na mazungumzo naye nafikiri kila kitu kinakwenda sawa tuache tufanye kazi,”alidokeza mmoja wa viongozi wa usajili wa Yanga akidai kwamba mchezaji huyo ameonyesha mzuka sana wa kuja Tanzania"