Mjumbe wa Kamati ya usajili Yanga Injinia Hersi Said amefunguka kuhusu mpango mkakati wa Yanga kumaliza msimu huu wakiwa mabingwa na maboresho ya kikosi kuelekea msimu ujao
Msimu huu umebaki takribani miezi miwili kumalizika huku Yanga ikiwa na baadhi ya wachezaji waoamaliza mikataba
Injinia Hersi amesema lengo la kwanza ni kuhakikisha wanatwaa ubingwa, wachezaji ambao Kocha Nasreddine Nabi atapendekeza kuendelea nao msimu ujao, wataongezewa mikataba
"Ni sahihi wapo wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwisho wa msimu na wangine ni miongoni mwa chachu ya mafanikio yetu sasa"
"Lakini Hatutakurupa, kama unavyoona malengo yetu sasa ni taji, hivyo kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi tunatakiwa kuwa na mastaa ambao watatubeba kwenye michuano hiyo," alisema Hersi
Hersi amesema usajili wao kuelekea msimu ujao utazingatia wachezaji ambao hawana majeraha ya mara kwa mara ili kuendana na kasi kama watapata nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa