Yanga imethibitisha kuwa winga Jesus Moloko ameanza mazoezi mepesi baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti hivi karibuni
Moloko anaweza kuwa tayari kuwakabili Simba April 30 katika mchezo ambao Yanga inazihitaji alama zote ili kusafisha njia kuelekea ubingwa wa 28 wa ligi kuu
Moloko wiki hii anafanya mazoezi chini ya uangalizi wa daktari wa Misuli, Youssef Ammar Mohamed ambapo nyota huyo atafanya program maalum ya mazoezi kwa wiki mbili
Aidha Youssef amedokeza kuhusu majeraha ya Khalid Aucho akibainisha kuwa nyota huyo tayari amepona, ameanza mazoezi ya utimamu wa mwili ambayo ataendelea nayo katika timu ya Taifa ya Uganda
Kuhusu Saido Ntbazonkiza, Youssef amesema nyota huyo alipewa mapumziko ili apone jeraha la goti na pia walimpa ruhusa ya kufunga ndoa Jumamosi iliyopita
Saido ameanza mazoezi huko Burundi na atarejea baada ya kumaliza muda wa 'fungate'
Abdallah Shaibu 'Ninja' ni nyota mwingine wa Yanga ambaye yuko katika 'fungate' baada ya kuoa Ijumaa iliyopita
Youssen amesema hata Chrispine Ngushi anakamilisha program ya mazoezi ya 'fitness' akitarajia kurejea kikosini wiki hii
Yacouba Songne ndiye mchezaji pekee ambaye anaweza kuendelea kukosekana mpaka mwezi Juni akiendelea na program maalum ya kumuimarisha baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa goti mwezi Novemba mwaka 2021