Mlinda lango wa Yanga, Djigui Diarra amejumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Mali ambacho kitacheza mechi mbili za hatua ya mwisho ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu dhidi ya Tunisia, Machi 25 na 29.
Kocha Mohamed Magassaouba amemjumuisha Diarra katika kikosi hicho cha wachezaji 28 ambacho kitakuwa na makipa watatu wakiwemo pia Ibrahim Mounkoro anayedakia TP Mazembe na Ismael Diawara wa Malmo ya Sweden.
Beki na nahodha wa timu hiyo, Hamari Traore wa Stade Rennes ya Ufaransa ataongoza jeshi hilo la nyota 28 lenye mastaa wengi wanaocheza soka la kulipwa katika ligi kubwa za soka barani Ulaya
ADVERTISE HERE