Wachezaji sita wa Yanga walioitwa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', wameingia kambini jana na wenzao kuelekea michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Afrika ya Kati na Sudan
Mechi hizo zitapigwa Machi 23 na Machi 29 yakiwa ni mashindano maalum yanayohusisha mataifa ya Tanzania, Sudan na Afrika ya Kati. Mechi zote zinapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Aboutwalib Mshery, Farid Mussa, Bakari Nondo Mwamnyeto, Dickson Job, Feisal Salum na Zawadi Mauya wamejumuishwa katika kikosi cha Kim Poulsen wakati kiungo Khalid Aucho ameitwa timu ya Taifa ya Uganda
Aidha wachezaji Yannick Bangala na Djuma Shabani wao watabaki nchini kwani hawakujumuishwa kwenye kikosi cha mwisho cha DR Congo ambacho kinawania nafasi ya fainali za kombe la dunia dhidi ya Morocco mechi zikipigwa Ijumaa Machi 25 na Jumanne ya Machi 29