Yanga kuivaa Azam FC kwa tahadhari kubwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
27 Jan 2018
Yanga kuivaa Azam FC kwa tahadhari kubwa
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, amekiri mchezo wao wa leo dhidi ya Azam FC utakuwa mgumu kutokana na kukosekana kwa baadhi ya nyota wake wa kikosi cha kwanza.

Yanga leo itakuwa ugenini kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi kuikabili Azam FC iliyo na rekodi ya kutofungwa ikiwa inacheza kwenye uwanja wake.

Kwenye mchezo huo Yanga inawakosa mshambuliaji wake, Amissi Tambwe, Thaban Kamusoko, Pius Buswita na Pato Ngonyani.

Wengine ni Donald Ngoma, Abdallah Shaibu 'Ninja' na Yohana Nkomola.

Tambwe ambaye alianza mazoezi na timu yake wiki hii, juzi alijitonesha tena kwenye mguu wake na hivyo atakosekana katika mchezo wa leo ambao unakamilisha mzunguko wa kwanza.

Licha ya kukosekana kwa wachezaji hao, Lwandamina amesema timu imejiandaa kupambana kwa ajili ya kuvuna pointi tatu.

“Hatutakuwa na Tambwe, Buswita pia Kamusoko naye hajawa fiti, lakini tutapambana, tunawaheshimu Azam lakini hatuwahofii,” alisema Lwandamina.

Kukosekana kwa Buswita, bado kunamfanya Mzambia huyo kumpanga Raphael Daudi au Saidi Makapu kwenye kiungo, atakayecheza pamoja na mkongo Papy Tshishimbi.

Kwa upande wake, Kocha wa Azam FC, Aristica Cioaba, alisema kuwa atatumia udhaifu aliouona kwenye kikosi cha Yanga kuweza kupata ushindi kwenye mchezo huo ambao unahusisha timu zinazowania ubingwa.

“Nina kikosi imara, tupo tayari kukabiliana na Yanga na sina shaka, Yanga ni timu kubwa, lakini hilo halitusumbui kwa sababu mpira unachezwa uwanjani, tusubiri dakika 90,” alisema kocha huyo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →