Mchezo wa mapema, Yanga Princess ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ilala Queens, mchezo ambao ulitumika kumuaga mshambuliaji Aisha Masaka ambaye amesajiliwa na timu ya ligi kuu Sweden
Mchezo wa pili kati ya viongozi wa Yanga dhidi ya Wasanii umemalizika kwa viongozi wa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-1

Mohammed Hussein 'Mmachinga' amekumbushia enzi zake akiifungia Yanga bao la kusawazisha kabla Injinia Hersi Said kuweka kambani bao la ushindi
Ilikuwa na shamra shamra kuwashuhudia wasanii na viongozi wa Yanga wakiupiga mwingi dimba la Mkapa
Haji Manara nae alipata nafasi ya kukonga nyoyo za mashabiki
Burudani zinaendelea uwanja wa Benjamin Mkapa kuelekea mchezo dhidi ya KMC saa moja usiku


ADVERTISE HERE