Hii ni siku kubwa kwa wapenzi, wanachama na mashabiki wa Yanga kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa kuanzia saa moja usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Lakini pia ni siku kubwa kwa Watanzania wote ambao wanaadhimisha mwaka mmoja wa uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Mama Samia Suluhu Hassan kilele cha tukio hilo ni uwanja wa Benjamin Mkapa mgeni wa heshima akiwa Rais wa Awamu ya Nne Mh Dk Jakaya Mrisho Kikwete
Ni heshima kubwa kwa Yanga kunogesha tukio hilo, wakati ni huu sasa Wananchi tuelekea uwanja wa Benjamin Mkapa
Mchezo unapigwa saa moja lakini kutakuwa na burudani 'kibaooo' za utangulizi
ADVERTISE HERE