Yanga 'kunogesha' mwaka mmoja wa Mama Samia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Mar 2022
Yanga 'kunogesha' mwaka mmoja wa Mama Samia

Leo Machi 19 2022, ni kilele cha Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia katika uongozi wa Taifa hili tarehe kama ya leo mwaka 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dk John Magufuli

Yanga imeungana na Watanzania wote wanaoadhimisha siku hii kwa kuandaa matukio mbalimbali ambayo yatahitimishwa pale uwanja wa Benjamin Mkapa kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC

Asubuhi kuna zoezi la kufanya usafi ndani ya Jiji la Dar es salaam ambapo viongozi, wanachama na mashabiki wa Yanga watafanya usafi Makao Makuu ya klabu hiyo yaliyo katika mitaa ya Twiga na Jangwani

Baadae shamrashamra zitaelekea uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo kutakuwa na burudani za aina mbalimbali kutoka kwa wasanii ikiwa ni pamoja na michezo ya utangulizi

Kina dada wa Yanga Princess wakichuana na wenzao wa Ilala Queens. Pia kutakuwa na mchezo kati ya Viongozi wa Yanga wakiunda timu pamoja na wadhamini wao dhidi ya Wasanii wa sanaa zote wakiwa pia wameunda timu yao

Shamrashamra zitakazojiri uwanja wa Benjamin Mkapa leo hazina tofauti na zile zinazojili kwenye matukio ya kilele cha wiki ya Mwananchi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’