Uongozi wa klabu ya Yanga umewata wapenzi na Wanachama wake kujitokeza kwa wingi leo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo ya mifupa kwa ajili ya kuchangia damu
Katika maadhamisho ya mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya sita Mh Samia Suluhu Hassan, Yanga imeandaa matukio mbalimbali ambayo kilele chake ni Jumamosi pale uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC
Moja ya matukio hayo ni hili la kuchangia damu ambapo Yanga pia imewataka viongozi wa Matawi kuhakikisha zoezi hilo linafanyika Tanzania nzima
Kuanzia saa mbili asubuhi zoezi litaanza Hospitali ya Muhimbili ambapo watu 200 wa kwanza watazawadiwa jezi za Yanga
ADVERTISE HERE