Kikosi cha Yanga kiko tayari kuikabili Azam FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom unaotarajiwa kupigwa kesho Jumamosi Januari 27 kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi.
Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika.
"Kila kitu kimekamilika kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Azam Fc,tunaiheshimu sana Azam kwani wamekuwa na msimu mzuri wanapata matokeo ndani na nje ya uwanja wao wa nyumbani.
"Ila hata sisi tupo vizuri na tunatarajia kupata matokeo kwenye mchezo wa kesho," Ten amewaambia waandishi wa habari leo.
Aidha Ten amesema wachezaji saba wa Yanga wanatarajiwa kukosa mchezo huo kutokana kuwa majeruhi.
"Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Azam FC wachezaji saba wataukosa mchezo huo Yohana Mkomola,Pius Buswita,Thaban Kamusoko,Amissi Tambwe,Abdallah Shaibu,Donald Ngoma na Pato Ngonyani ambao wote wote ni wagonjwa.
"Aidha, pamoja na kuumwa Pius Buswita anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano."
Wakati huo huo, Dismas Ten amesema uongozi wa Yanga umekamilisha taratibu zote za kuhuisha kibali cha kocha Mkuu George Lwandamina.
"Kuhusu swala la kibali cha Mwalimu tayari kimefanyiwa kazi na taratibu zote zimeshafuatwa ivyo mashabiki na wanachama waondoe shaka juu ya jambo hilo."
Katika michezo mitatu iliyopita, Lwandamina amelazimika kukaa jukwaani kutokana na kutokuwa na kibali cha kufanya kazi nchini baada ya kile cha awali kuisha muda wake.

ADVERTISE HERE