Winga Jesus Moloko ameanza mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa daktari ikiwa ni program ya awali kuelekea kurejea uwanjani
Moloko alifanyiwa upasuaji mdogo katika goti lake la mguu wa kushoto baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Biashara United

Winga huyo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Yanga msimu huu akifunga mabao matatu na kutoa pasi mbili za mabao
Tayari amekosekana kwenye kikosi cha Yanga kwa takribani wiki nne nafasi yake ikichukuliwa na kinda Denis Nkame ambaye taratibu amenza kuingia katika mfumo wa kocha Nasreddine Nabi
Idadi ya majeruhi kwenye kikosi cha Yanga imeendelea kupungua ambapo mpaka sasa wachezaji wote waliokuwa majeruhi wanaendelea na program za mazoezi kurejesha utimamu wa miili yao huku wengine wakiwa tayari wamerejeshwa kikosini