Jana Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Kim Poulsen alimjumuisha winga wa Yanga Farid Mussa katika kikosi chake ambacho kitacheza mechi za Kimataifa za kirafiki kwenye kalenda ya FIFA
Poulsen alibainisha kuwa alivutiwa na ubora wa Farid alioonyesha kwenye kikosi cha Yanga pale alipotumika kama mlinzi wa kushoto
Kwa miaka yote ambayo Farid ameitwa timu ya Taifa, alikuwa akitumika kama kiungo wa ushambuliaji au winga lakini kwa mara ya kwanza huenda akatumika kama mlinzi wa kushoto
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ndiye aliyefichua kipaji cha Farid katika safu ya ulinzi upande wa kushoto
Baada ya mfululizo wa majeruhi ndani ya kikosi, Nabi alilazimika kumbadili Farid na kwa hakika ulikuwa uamuzi sahihi kwani kwa sasa kuna kila dalili Farid anaweza kuwa chaguo la kwanza nafasi ya ulinzi upande wa kushoto
Ni fursa nyingine imefunguka kwa Farid kwa timu ya Taifa, kumshawishi Poulsen na pengine kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza