Yanga yatangaza kuanza kwa mchakato wa uchaguzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Mar 2022
Yanga yatangaza kuanza kwa mchakato wa uchaguzi

Klabu ya Yanga imetangaza kuanza kwa mchakato wa uchaguzi Mkuu wa mwaka wakianza na uchaguzi wa Matawi

Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo, Mtendaji Mkuu wa Yanga Senzo Mazingisa amesema baada ya Mabadiliko ya Katiba ya Yanga ya mwaka 2021 kuidhinishwa na Serikali, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa hadi Juni 30 Yanga iwe imebadili muundo wake kulingana na Katiba

Senzo amesema walianza kwa kuandikisha Matawi ambapo waliweka vigezo ili Tawi liweze kutambulika linapaswa kuwa na Wanachama wasiopungua 100 ambapo Matawi yaliyokidhi vigezo yamekabidhiwa vyeti vya kutambuliwa

Aidha Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Malangwe Ally Mchungahela ametangaza March 18 matawi yote yaliyokidhi vigezo yaanze chaguzi za kupata viongozi wake

Mchungahela amesema Matawi yatafanya Uchaguzi kuanzia March 18 mpaka mwishoni mwa mwezi April kabla ya kufanyika uchaguzi wa viongozi wa Juu

Nafasi ambazo zitawaniwa kwenye Matawi ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu wa Tawi, Mweka Hazina na Wajumbe Wanne

Viongozi wa juu wa Tawi (Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Mwekahazina) pamoja na Wajumbe wawili watawakilisha Tawi katika uchaguzi wa kupata viongozi wa juu wa klabu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’