Wananchi leo wana jambo lao uwanja wa Azam Complex katika mchezo wa hisani dhidi ya timu ya Taifa ya Somalia
Ni mchezo maalum wa kuchangia fedha kwa ajili ya taasisi ya Ali Kimara kusaidia watoto wenye matatizo maalum
Ni mchezo wa aina yake ambao mashabiki wataushuhudia pale Azam Complex, mtanange huo unatarajia kuwa na upinzani mkali
Yanga kucheza na timu ya Taifa ni heshima kubwa kwao hivyo watahakikisha wanashinda mchezo huo kuwapa furaha mashabiki wao
Somalia nao hawatapenda kufungwa katika mchezo huo, hasa wakiwa na hadhi ya timu ya Taifa
Ni mchezo ambao Kocha Nasreddine Nabi anatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake akiwapa nafasi nyota wengine hasa wale wanaorejea kutoka katika majeruhi
Pengine leo Wananchi wanaweza kumshuhudia mshambuliaji Chico Ushindi akirejea kikosini baada ya kupona maradhi
Mchezo utapigwa kuanzia saa moja usiku..
Β