Katika mazoezi ya jana benchi la ufundi la Yanga liliweka mkazo zaidi kwenye safu ya ushambuliaji kuhakikisha inatumia nafasi ipasavyo.
Yanga inajiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Azam FC.
Mchezo huo utapigwa kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi kesho Jumamosi, Januari 27.
Mbali na kuboresha safu ya ushambuliaji, umiliki wa mpira na umaliziaji wa krosi ni mambo mengine yaliyowekewa mkazo katika mazoezi hayo.
Kwenye mchezo huo Yanga itakuwa na huduma ya mshambuliaji wake Obrey Chirwa ambaye amemaliza adhabu ya kukosa michezo mitatu.
Lakini itamkosa winga wake Pius Buswita anayetumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja baada ya kutimiza kadi tatu za njano.
Kelvin Yondani naye amemaliza adhabu ya kukosa mchezo mmoja huku winga Geofrey Mwashiuya akirejea kikosini baada ya kupona maradhi.

ADVERTISE HERE