Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema mchezo wa Kimataifa wa kirafiki wanaocheza dhidi ya Somalia utakuwa na ushindani mkali kwani timu ya Taifa hilo imeimarika
Manara amesema kikosi cha Somalia kitakachoshuka uwanja kesho Jumamosi kuikabili Yanga katika mchezo wa hisani, kitajumuisha wachezaji watatu tu wanaocheza ligi ya ndani
Amesema idadi kubwa ya wachezaji wa timu hiyo wanacheza ligi za Ulaya na Marekani
"Hawa Somalia tutakaocheza nao sio wale ambao tulikuwa tukiwafunga mpaka mabao 10. Wameimarisha sana timu yao, kutokana na sera ya uraia wa nchi hiyo, wamewapa uraia wachezaji wengi ambao hawakuzaliwa Somalia. Wamewekeza sana katika timu yao, ni kama ilivyokuwa kwa Comoro ambao miaka michache nyuma walikuwa 'vibonde', " alisema Manara
Somalia watacheza mechi mbili za Kimataifa za kirafiki ambapo pia watacheza na timu ya Taifa ya Swaziland