Nyota wa RS Berkane Tuisila Kisinda na Fiston Abdulrazak wametua leo jijini Dar es salaam wakiwa na kikosi cha RS Berkane ambacho Jumapili kitacheza na Simba kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika
Mshambuliaji Fiston Mayele na winga Jesus Moloko wakapata nafasi ya kuwatembelea maswaiba wao hao ambao msimu uliopita walikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga
Kisinda, Mayele na Moloko waliwahi kucheza pamoja katika klabu ya AS Vita
Pamoja na kuondoka nchini, Kisinda na Fiston bado wanaonyesha kuwa na mapenzi makubwa na Yanga
Katika moja ya mahojiano yake, Kisinda aliweka bayana kuwa kama mabosi wa Yanga watamuhitaji yuko tayari kurejea
ADVERTISE HERE