Leo zimeibuka tetesi kuhusu mshambuliaji kinara wa mabao ligi kuu ya NBC Fiston Mayele kuwa anawindwa na klabu ya Kaizer Chiefs
Hata hivyo Yanga haijapokea ofa yoyote kutoka kwa Kaizer Chiefs kumtaka mchezaji huyo
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema tetesi hizo ambazo zimeanzishwa kimkakati haziwezi kuwaondolea Wananchi focus yao kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu msimu huu
"Basi leo simu zote za waandishi ni kuhusu Mayele kwenda Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini. Ninachoweza kuwahakikishia ni kwamba anakwenda Avic Town," aliandika Bumbuli kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Mayele amepachika mabao 10 ligi kuu ya NBC msimu huu akiongoza mbio za kuwania kiatu cha dhahabu akiwa sambamba na Reliants Lusajo wa Namungo Fc
ADVERTISE HERE