Kadi ya njano aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold, inamfanya kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' akose mchezo unaofuata wa ligi kuu dhidi ya KMC ambao utapigwa March 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Sure Boy amefikisha kadi tatu za njano ambapo pia alionyesha kadi za njano katika michezo dhidi ya Mtibwa Sugar na Biashara United
Hata hivyo kiungo Khalid Aucho anatarajiwa kurejea kikosi kwenye mchezo dhidi ya KMC baada ya afya yake kuimarika kama ilivyo kwa Saido Ntibazonkiza, Djuma Shabani na Chico Ushindi
Kiwango bora alichoonyesha katika michezo iliyopita, kimemfanya Sure Boy ajihakikishie nafasi kwenye kikosi cha kocha Nasreddine Nabi
Sure Boy atarejea kikosini kuwakabili waajiri wake wa zamani Azam Fc katika mchezo utakaopigwa Azam Complex, April 06