Yanga inaweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu kama itafanya vizuri katika michezo saba inayofuata kwenye ligi kuu ambayo itapigwa jijini Dar es salaam
Yanga haitakuwa na mechi nyingi nje ya jiji la Dar katika duru ya pili baada ya kucheza asilimia kubwa ya mechi hizo kwenye duru ya kwanza
Kama Ruvu Shooting hawatahamisha mchezo dhidi ya Yanga ambao ratiba inaonyesha utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, May 04, Yanga itakuwa imesalia na michezo mitatu tu nje ya Dar es salaam dhidi ya Biashara United, Mbeya City na Dodoma Jiji
Katika michezo saba inayofuata, mchezo mmoja utapigwa uwanja wa Azam Complex, dhidi ya Azam Fc na mechi sita kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
March 16 Wananchi watakuwa kwa Mkapa kuikabili KMC na baadae kuelekea Chamazi kuikabili Azam FC April 06
April 30 Yanga itarejea uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Simba katika mchezo muhimu ambao ushindi kwa Yanga utawasogeza karibu na ubingwa
May 04 Wananchi watarudi tena uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Ruvu Shooting ambapo baada ya mchezo huo, Yanga itakuwa na mechi tatu mfululizo katika uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Namungo Fc, Tanzania Prisons na Mbeya Kwanza
Hizi ni mechi saba muhimu kwa Yanga ambazo zinaweza kutosha kuwafanya Wananchi wakawa mabingwa wa ligi kuu msimu huu