Mayele azawadiwa ng'ombe mwingine Mwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Mar 2022
Mayele azawadiwa ng'ombe mwingine Mwanza

Mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele jana aliondoka na zawadi ya ng'ombe mkoani Mwanza baada ya kufunga bao pekee la ushindi dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba

Ni zawadi kutoka Tawi la Yanga kutoka Kahama, mkoani Shinyanga. Huyo ni ngo'mbe wa pili Mayele anazawadiwa na mashabiki wa Yanga msimu huu

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema klabu inafanya utaratibu wa kumsafirisha ngo'ombe huyo jijini Dar es salaam. Thamani ya ng'ombe huyo ni Tsh 750,000/-

Mayele alizawadiwa ngo'mbe wa kwanza mkoani Morogoro baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar akifunga bao la pili katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0

Katika hatua nyingine, Bumbuli amewatoa hofu mashabiki wa Yanga kuhusu hali ya Mayele ambaye jana alipata majeraha na kushindwa kumaliza mchezo dhidi ya Geita Gold

Bumbuli amesema Mayele anaendelea vizuri ambapo madaktari wamesema atahitaji siku tatu kupumzika kabla ya kurejea tena uwanjani

Hivyo Mayele atakuwepo uwanja wa Benjamin Mkapa wakati Yanga itakapoikaribisha KMC katika mchezo utakaopigwa March 16

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’