Ni ushindi wa jasho na damu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Mar 2022
Ni ushindi wa jasho na damu

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema mchezo wa leo dhidi ya Geita Gold ulihitaji mbinu zaidi kwani walihitaji ushindi licha ya changamoto zilizokuwa zikiwakabili

Katika mchezo huo bao la Fiston Mayele alilofunga kwenye sekunde ya 30, liliihakikishia Yanga alama tatu muhimu zinazowaweka kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 11

Takwimu za dakika 90 za mchezo huo, zinaonyesha Geita Gold walikuwa na umiliki zaidi wa mpira kuliko Yanga

Nabi amesema baada ya kupata bao la mapema, walijua Geita Gold wangekuja juu kusaka bao la kusawazisha hivyo walilazimika kucheza kwa nidhamu zaidi katika kujilinda

Aidha Nabi amesema kukosekana kwa baadhi ya wachezaji, ilimlazimu kubadili mbinu za mchezo huo ili kuhakikisha wanatimiza malengo ya kupata ushindi

"Tulifunga goli la mapema ambalo liliwafanya Geita kuanza kushambulia zaidi, nikaamua kuipanga timu yangu icheze kwa kulinda ushindi ili kupata alama tatu muhimu"

"Tuna majeruhi wengi na imefika wakati wa kucheza kimbinu kusaka ushindi," alisema Nabi ambaye leo ametangazwa kuwa kocha bora wa ligi kuu kwa mwezi Februari 2022

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’