Waamuzi walinde afya za wachezaji - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Mar 2022
Waamuzi walinde afya za wachezaji - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema pamoja na kutambua ugumu wa ligi kuu ya NBC msimu huu, bado waamuzi wana jukumu la kulinda afya za wachezaji

Nabi ametoa kauli hiyo kufuatia mfululizo wa majeruhi yanayoikumba klabu ya Yanga katika kila mchezo ambapo mpaka sasa wachezaji takribani saba ni majeruhi

Nabi amesema anatambua kwamba Ligi ni ngumu na timu nyingi zinapambana kupata matokeo hivyo kutokea migongano mingi baina ya wachezaji inayosababisha majeraha lakini anashangazwa kwanini katika kila mchezo nyota wake zaidi ya wawili lazima waumie majeraha yanayowaweka nje muda mwingi

"Tunafahamu Ligi imekuwa ngumu wachezaji wanajitoa sana kusaka ushindi kwahiyo migongano inatokea ni jambo la kawaida, lakini kwanini inatokea sana kwa wachezaji wetu tazama mchezo huu tunakosa wachezaji wengi muhimu ukiacha Shaban na Ushindi ambao wana Malaria"

"Kwahiyo tunaomba waaamuzi walinde wachezaji siyo wa Yanga tu bali wawalinde wachezaji wote na kuwaepusha na haya maaumivu yanayozigharimu timu zao," alisema Nabi

Nabi amethibitisha kuwa wachezaji Khalid Aucho na Saido Ntibazonkiza nao watakosekana katika mchezo dhidi ya Geita Gold baada ya kupata majeraha

Wanaungana na Chrispine Ngushi, David Bryson na Yacouba Songne ambao bado wako nje wakiendelea kuimarika huku Ushindi na Shabani Djuma wakiwa wagonjwa

Pamoja na kuwakosa wachezaji hao, kocha msaidizi wa Yanga Cedrick Kaze amesema kikosi chao kiko imara kuzisaka alama zote tatu dhidi ya Geita Gold

"Hatuwezi kuyumba kwa kuwakosa wachezaji hao kwani walishakosekana katika michezo iliyopita na tukashinda. Ni jukumu letu benchi la ufundi kuangalia nani wanaweza kuchukua nafasi zao kwani tuna wachezaji wengi wazuri," alisema Kaze

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’