Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam leo kuelekea Mwanza wanakokabiliwa na mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Geita Gold
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumapili, March 06 katika uwanja wa CCM Kirumba
Wananchi wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 11, wanazihitaji alama zote tatu katika mchezo huo ili kuendelea kujiimarisha katika mbio za kuwania ubingwa msimu huu
Matokeo ya kila mchezo katika duru ya pili yana umuhimu wa kipekee kwani hii ni hatua ya lala salama
ADVERTISE HERE