Majeraha yalimchelewesha Saido Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Mar 2022
Majeraha yalimchelewesha Saido Yanga

Kocha Msaidizi wa Yanga Cedrick Kaze amesema kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza amekuwa katika kiwango bora baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimsumbua mara kwa mara

Ntibazonkiza alisajiliwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili msimu uliopita lakini muda mwingi alkaa nje kutokana na majeraha hayo

Tangu kuanza kwa msimu huu Saido ameimarika na sasa amejihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza, akionyesha thamani yake kikosini

Amehusika katika mabao 10 yaliyofungwa na Yanga kwenye ligi akifunga mabao sita na kutoa pasi nne za mabao

Ukimtoa Fiston Mayele ambaye amehusika katika mabao 12, anayefuata ni Saido

Kaze amesema Saido ni mzoefu wa ligi za Afrika hivyo akiwa fiti kifiziki amekuwa akifanya mambo ya tofauti sana uwanjani akishirikiana na wenzie wanaomwelewa vilivyo kuanzia mazoezini

"Saido akiwa vizuri kwenye fiziki ni mchezaji mzuri sana, ana akili ya mpira na anajua kuamua mechi. Yeye na wenzake wana morali kubwa ya kupigania mafanikio na kulinda hadhi ya Yanga. Bado tuna mwendo mrefu lakini angalau njia inaonekana kufikia mafanikio," alisema kaze

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’