Kocha Azam FC atamba atafunga kila timu VPL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jan 2018
Kocha Azam FC atamba atafunga kila timu VPL
Kocha Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, amesema kuwa timu yake inafanya mazoezi ya kushinda mechi zote za Ligi Kuu Tanzania Bara na kamwe si kuwavaa mabingwa watetezi , Yanga.

Azam FC itakuwa mwenyeji wa Yanga katika mechi ya ligi hiyo itakayofanyika keshokutwa kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi jijini Dar es Salaam.

Kwenye mahojiano yake na gazeti la Nipashe, Cioaba, amesema kuwa siku zote katika mipango yake anajiandaa kuzikabili timu zote 15 na si vinginevyo.

Cioaba alisema kuwa ili uweze kuwa bingwa ni lazima upate ushindi katika mechi nyingi na si moja dhidi ya Yanga au Simba na hilo linawajenga wachezaji wake kuheshimu timu zote zinazoshiriki ligi hiyo ya juu hapa nchini.

"Tunajiandaa kushinda mechi dhidi ya timu zote 15 zilizoko kwenye ligi, huwezi kuwa bingwa kwa kuifunga Yanga au Simba au Singida United, unatakiwa kupambana kupata pointi nyingi kwa kushinda mechi nyingi bila kuchagua jina la mpinzani," alisema kocha huyo.

Naye Msemaji wa timu hiyo, Jaffer Iddi, alisema jana kuwa mechi hiyo itachezwa saa kumi jioni kama ratiba ilivyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)

Aliongeza kuwa kikosi chao kinaendelea vyema na mazoezi na wanaufahamu ubora na ukubwa wa Yanga ambao watakutana nao Jumamosi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’