Kikosi cha Yanga kinaingia kambini leo kukamilisha maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold ambao utapigwa Jumapili, March 06 uwanja wa CCM Kirumba
Benchi la ufundi na wachezaji jana jioni walikuwa sehemu ya waomboleza waliohudhuria mazishi ya Mzee Said Mohammed, baba mzazi wa mdhamini wa Yanga, Ghlaib Said Mohammed
Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema kikosi kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam Ijumaa kuelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo huo ambao Wananchi wanazihitaji alama zote tatu
Habari njema kwa Yanga ni kurejea kwa baadhi ya wachezaji wake muhimu Feisal Salum 'Fei Toto' na Dickson Job ambao wamemaliza adhabu zilizokuwa zikiwakabili
ADVERTISE HERE