Mwanachama maarufu wa klabu ya Simba Mzee Muchacho jana alishindwa kujizuia mbele ya mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele na kuomba wapige picha
Mzee Muchacho alikuwa miongoni mwa waombolezaji waliofika katika mazishi ya Mzee Said Mohammed, baba mzazi wa mdhamini wa Yanga, Ghalib Said Mohammed
Muchacho amemuahidi Mayele zawadi ya Mbuzi kama ataweza kufunga katika mchezo dhidi ya Simba kwenye ligi au kombe la FA kama timu hizo zitakutana katika hatua ya nusu fainali
"Nimekutana na Mayele, tumepiga picha, nimemuahidi zawadi ya mbuzi kama atatufunga (Simba) kwenye mchezo wa ligi au kombe la FA," alisema Muchacho
Hivi karibuni Mayele alizawadiwa ng'ombe mkoani Morogoro baada ya kufunga bao kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa uwanja wa Manungu, Turiani