Licha ya vipigo wanavyogawa kwenye ligi kuu ya NBC, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema bado timu haijafika katika ubora anaoutaka
Mwanzoni mwa msimu Nabi aliomba siku 90 (miezi mitatu) kukisuka kikosi cha Yanga pale walipoondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kwa kufungwa na Rivers United
Licha ya mafanikio aliyopata mpaka sasa akiiongoza Yanga kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama 11, Nabi amesema bado timu haijafika anapotaka
"Ni kweli timu imeimalika lakini bado hatujafika kwenye kiwango ninachotaka, bado kuna kazi tunapaswa kuendelea kuifanya katika uwanja wa mazoezi," alisema Nabi
Msimu huu Nabi amepewa jukumu la kuhakikisha Yanga inatwaa ubingwa wa ligi kuu, mpaka sasa amefanikiwa kwa asilimia 50 na mapambano ya asilimia nyingine 50 yameanza vyema kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar juzi