Tusibweteke bado tuna kazi ya kufanya - Dk Msolla

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Mar 2022
Tusibweteke bado tuna kazi ya kufanya - Dk Msolla

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amewataka wapenzi, wanachama na mashabiki wa Yanga kutobweteka kutokana na mafanikio waliyopata katika duru ya kwanza ligi kuu ya NBC

Yanga ilifunga vyema duru ya kwanza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar na ikaanza duru ya pili kibabe kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar na kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu baada ya kufikisha alama 42

Yanga inaongoza ligi kwa tofauti ya alama 11 dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili

Dk Msolla amesema kama ni mechi wamecheza kipindi cha kwanza wanaongoza hivyo wanapaswa kurejea katika kipindi cha pili kulinda matokeo waliyopata na kufunga mabao zaidi

Amesema benchi la ufundi na wachezaji wana kazi ya kufanya katika michezo 14 iliyobaki ili kuhakikisha wanatwaa ubingwa

"Nawataka benchi la ufundi na wachezaji wasibweteke kwa mafanikio haya. Wachezaji wanapaswa kupambana kuhakikisha tunafanikisha malengo yetu"

"Kwa mashabiki pia tusibweteke, tujitokeze kwa wingi viwanjani kuwaunga mkono. Uongozi tulionao sasa ni wa kipindi cha kwanza. Sasa tumeingia kwenye kupindi cha pili na tunapaswa kuhakikisha tunalinda matokeo hayo"

"Tunahitaji kushinda ubingwa msimu huu lakini safari bado, tuhakikishe tunafanya vizuri katika michezo 14 iliyobaki ambayo minne tutacheza nje ya jiji la Dar es salaam na 10 tutacheza hapa Dar es salaam," alisema Dk Msolla

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’