Jana baada ya mchezo dhidi ya Kegera Sugar uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0, mshambuliaji wa Kagera Sugar Hamis Kizza Diego, aliyewahi kuitumikia Yanga kwa mafanikio makubwa, alimtaja kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' kuwa kwake yeye alikuwa nyota wa mchezo huo
Lakini pia mfungaji wa mabao mawili ya Yanga, Fiston Mayele naye hakusita kulitaja jina la Sure Boy akikiri kuvutiwa na ufundi wa nyota huyo aliyetua Yanga katika usajili wa dirisha dogo mwezi Januari 2022
Sure Boy amezungumzwa na wengi baada ya kiwango bora alichoonyesha tangu mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar na jana dhidi ya Kagera Sugar
Kwa hakika Sure Boy ni fundi kwelikweli hasa anapokutana na mafundi wenzake ndani ya kikosi cha Yanga
Huu ni wakati mbaya sana kukutana na Yanga, hakuna anayetamani kukutana na Wananchi wakati huu wakiwa katika ubora wao
