Mwashiuya kamili kuivaa Azam FC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jan 2018
Mwashiuya kamili kuivaa Azam FC
Winga Geofrey Mwashiuya amerejea kikosini baada ya kuwa nje kwa wiki kadhaa kutokana na kuugua ugonjwa wa Malaria.

Mwashiuya ameanza kujinoa na kikosi cha Yanga jana.

Kurejea kwa Mwashiuya ni habari njema kwa kikosi cha Yanga kinachojiandaa kuivaa Azam FC siku ya Jumamosi.

Kwenye mchezo huo Yanga haitakuwa na kiungo wake wa ushambuliaji, Pius Buswita atakayekosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.

Pia Yanga huenda ikamkosa mshambuliaji wake kinda Yohana Nkomola ambaye aliumia kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting Jumapili iliyopita.

Aidha kinara wa mabao kwenye kikosi cha Yanga Obrey Chirwa naye amerejea kikosini baada ya kukosekana kwenye michezo mitatu iliyopita akitumikia adhabu ya kufungiwa idadi hiyo ya michezo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’