Yanga imetoa orodha ya nyota tisa ambao watakosekana leo kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa moja usiku
Wachezaji Dickson Job na Feisal Salum wanakosekana kwa sababu wanatumikia adhabu ya kadi
Job anakamilisha adhabu ya kukosa michezo mitatu wakati Feisal ana kadi tatu za njano
Wachezaji saba ni majeruhi ambao ni Kibwana Shomari, Abdallah Shaibu, Chrispine Ngushi, Chico Ushindi, Yacouba Songne, David Bryson na Jesus Moloko
ADVERTISE HERE