Kiungo mshambuliaji wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto' amekuwa na wakati mzuri tangu ujio wa kocha Nasreddine Nabi
Huu unaweza kuwa msimu wake bora zaidi tangu alipojiunga na Yanga kutokana na mchango wake katika upatikanaji wa mabao
Feisal amefunga mabao manne na pia kutoa pasi nne za mabao akihusika katika mabao nane kati ya 25 yaliyofungwa na Yanga
Feisal ndiye kinara wa kutoa pasi za mabao kwenye kikosi cha Yanga lakini pia yeye ni mchezaji wa pili kuhusika na mabao mengi ndani ya kikosi cha Yanga msimu huu
Ni Fiston Mayele aliyehusika na mabao mengi zaidi msimu huu akifunga mabao saba na kutoa pasi mbili za mabao akishiriiki katika upatikanaji wa mabao tisa
Kesho Jumapili Yanga inaanza duru ya pili kwa kuikaribisha Kagera Sugar katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Kwenye mchezo wa duru ya kwanza, ni Fei Toto alyeihakikishia Yanga alama tatu muhimu kwa ushindi wa bao 1-0 kule Kaitaba, Kagera