Ametetema tena! Ndio! Fiston Mayele ametetema uwanja wa Manungu akifunga bao lake la saba msimu huu. Mayele alifunga bao la pili la Yanga katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar
Lakini huwezi kuzungumzia ushindi huo muhimu wa Yanga pasipo kumtaja Saido Ntibazonkiza 'God father' ambaye kwa hakika alikuwa nyota wa mchezo huo
Alifunga bao la kwanza la Yanga mwishoni mwa kipindi cha kwanza akimalizia pasi murua ya Feisal Salum 'Fei Toto' aliyenyang'anya mpira katika eneo la kiungo
Saido alitengeneza bao la pili la Fiston ambalo limemfanya aondoke Manungu na zawadi ya ngo'mbe kutoka kwa shabiki aliyefika mahsusi kumshuhudia pamoja na kocha Nasreddine Nabi
Ulikuwa mchezo ambao Yanga ingeweza kufunga mabao zaidi kutokana na idadi ya nafasi nyingi walizotengeneza
Feisal alifunga bao ambalo hata hivyo halikuwa sahihi kwani aligusa mpira kwa mkono katika harakati za kuweka mpira kimiani
Yanga imefikisha alama 39, sasa wakiongoza ligi kwa tofauti ya alama nane
Wananchi wanakwenda kuanza mzunguuko wa pili wakiwa na faida ya alama nane kibindoni





