Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Yanga, Hussein Nyika amesema zoezi la usajili linakwenda vizuri na huenda Jumamosi wachezaji wengine waliosajiliwa watawekwa hadharani.
Akizungumza kwa kujiamini Nyika amesema siku hiyo Yanga itatangaza usajili mzito ambao yeye aliufananisha na bomu la nyuklia.
Amesema usajili wa mwaka huu umelenga kutengeneza kikosi imara kitakachofanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa kwani klabu inahitaji ushindani mpya baada ya kutawala sana ligi ya Vodacom.
Yanga imedhamiria kukamikisha zoezi la usajili mapema ili wachezaji wapya wapate muda wa kuzoea mifumo ya mwalimu.
Dirisha la usajili litafungwa Agosti 06, 2017 na TFF tayari imetahadharisha kuwa hakuna muda wa ziada utakao ongezwa baada ya tarehe hiyo kupita.

ADVERTISE HERE