Mlinzi wa Yanga Yanga Kibwana Shomari amewashukuru wapenzi, wanachama na mashabiki kwa kumuombea mema katika kipindi alichokuwa majeruhi
Aidha Kibwana ameushukuru uongozi wa Yanga na wadhamini GSM kwa kuhakikisha anapata matibabu sahihi yatakayo mrejesha uwanjani mapema
Kibwana alipata majeraha kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba uliopigwa Disemba 11 na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana
Katika mchezo huo Kibwana alifanya kazi kubwa katika nafasi yake ya ulinzi wa kushoto ambako aliweza kuwadhibiti Kibu Denis (alitolewa), Bernard Morrison (alitolewa) na Yusufu Mhilu
Kiwana amesema alikuwa na hofu kuwa pengine majeraha hayo yangemuweka nje kwa muda mrefu na kumharibia mipango na ndoto alizokuwa nazo katika maisha yake ya kusakata kabumbu
"Hofu yangu kubwa ilikuwa kwenye upasuaji maana Nilikuwa sijawahi kufanyiwa upasuaji na kama kijana mdogo bado nina malengo na ndoto kubwa kwenye mpira," alisema Kibwana