Nabi ataka ushindi mnono dhidi ya Mtibwa Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Feb 2022
Nabi ataka ushindi mnono dhidi ya Mtibwa Sugar

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema malengo yake ni kuona timu yake inashinda mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Uwanja wa Manungu na kuweka rekodi ya kukamilisha mzunguko wa kwanza bila kupoteza

Yanga ipo kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 36, baada ya kushuka uwanjani mara 14, ambapo imefanikiwa kushinda michezo 11 na kutoka sare mara tatu pekee dhidi ya Simba, Namungo na Mbeya City.

Nabi amesema ili kutimiza malengo yao msimu huu ambayo ni kutwaa ubingwa, wanapaswa kushinda kila mchezo unaokuja mbele yao.

Amesema jambo rahisi lakini litawezekana kama kila mmoja ndani ya kikosi atatimiza wajibu wake.

"Tuna ratiba nzuri ambayo inatupa nafasi ya kujipanga zaidi kwa mechi zilizosalia ingawa tutawakosa baadhi ya wachezaji kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo majeraha na adhabu, lakini wachezaji waliobaki wanatosha kufanya kitu na kupata matokeo kwenye mechi hii, sisi benchi la ufundi tumeupa umuhimu mkubwa mchezo huu kuhakikisha tunashinda."

"Tunaenda kumkosa Dickson Job, sababu ya adhabu lakini pia tunaenda kuwakosa wachezaji zaidi ya watano, lakini nafurahi kurejea tena kwa Djuma Shaaban ambaye alikosa michezo mitatu iliyopita naamini ataongeza kitu kwenye mchezo ujao," alisema Nabi

Nabi amesisitiza kuwa haangalii uwezo wa timu ambazo anakwenda kukutana nazo bali anachokifanya ni kuhakikisha anawaandaa wachezaji wake kwa kuwajenga kimbinu na kisaikolojia ili waweze kupambana na kupata matokeo katika mechi za mashindano yote wanayoshiriki.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’