Mwanzoni mwa wiki ijayo, Yanga itasafiri mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa Jumatano, Februari 23 katika uwanja wa Mnungu, Turiani mkoani Morogoro
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wanahitaji kushinda mchezo huo ili kuhakikisha wanaendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi
Bumbuli amewataka wapenzi na wanachama wa Yanga kuwa wamoja kuelekea mchezo huo ili kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu mkoani Morogoro
Amesema mchezo huo hautakuwa kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga pekee, wanafahamu Mtibwa Sugar watapata sapoti kutoka kwa wapinzani wao Simba ambao dua zao ni kuona Yanga haiondoki na alama tatu Manungu
ADVERTISE HERE