VAR inakuja Ligi Kuu NBC

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Feb 2022
VAR inakuja Ligi Kuu NBC

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa amesema Serikali inakusudia kufunga machine za Kisasa za kufuatilia mchezo (VAR) ili kuondoa Changamoto zinazojitokeza Wakati mchezo Ukiendelea.

Mchengerwa ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam leo alipokutana na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF.

"Tunajipanga kuwa na vyombo vya Ufuatiliaji wakati mchezo ukiendelea, tutaanza na viwanja vitano ukiwa ni mpango wa Serikali ambao tumeufikiria kwa Sababu tunaenda kufanya maboresho ya miundombinu kwenye viwanja vyetu," amesema Mchengerwa

Aidha Waziri Mchengelwa amesema Serikali imeliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na TFF wamalize changamoto ya waamuzi wanaochezesha pasipo kufuata maadili ya kazi yao

"Kamati inayohusika na Waamuzi ijitafakari, hili suala tunawaachia TFF walimalize, lakini kama Wizara tunaiagiza BMT kukaa pamoja na TFF ili kuangalia namna ya kuondoa changamoto ya Waamuzi ambao hawazingatii Maadili"

"Pia TFF iandae Semina kwa Waamuzi wa mpira wa miguu ambapo pia Wenzetu wa Takukuru nao wawepo ili kutoa Elimu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’