Walichofanya mashabiki wa Simba kuwashambulia Yanga ni ushamba tu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Feb 2022
Walichofanya mashabiki wa Simba kuwashambulia Yanga ni ushamba tu

Jana wapo mashabiki wa Yanga ambao waliingia uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Simba dhidi ya Asec Mimosas

Wapo walioingia kwa lengo la kuwaunga mkono Asec Mimosas, ni kawaida shabiki kindakindaki wa Yanga haitakuwa rahisi kwake kwenda uwanjani kuishangilia Simba kutokana na historia na upinzani wa jadi uliopo baina ya timu hizo kongwe zaidi hapa Tanzania

Iko hivyo hata kwenye michezo ya Yanga utawakuta mashabiki wa Simba wengi tu wakishangilia timu pinzani

Zipo video zinaonyesha mashabiki wa Simba wakiwashambulia majukwaani mashabiki wa Yanga waliokuwa wamevaa jezi zao. Ni aibu kuona matukio ya aina hii yanaendelea viwanjani

Ukiwasikiliza viongozi wa Simba wanatamba kuwa mashabiki wao ni bora zaidi nchini kwa sababu ni waungwana, waliopevuka kiakili

Ubora huo ni ule wa kupiga wenzao bakora kwa sababu tu hawaungi mkono timu yao?

Mbaya zaidi wanapiga wenzao katika mchezo ambao camera za CAF zinachukua kila tukio

Kama CAF watachukulia tukio lile kwa 'userious' ni wazi Simba inaweza kuadhibiwa na hata kuzuiwa kuingiza mashabiki katika michezo yao

Zipo nyakati misimu kadhaa iliyopita mashabiki wa Yanga walituhumiwa na hata baadhi yao kufungiwa kwenda viwanjani kwa matukio ya aina hiyo

Naamini mamlaka zimeona tukio lile, wanapaswa kuchukua hatua kwani hii sio mara ya kwanza kwa mashabiki wa Simba kuwashambulia wenzao wa Yanga

Soka ni mchezo wa kiungwana, ipo siku yatatokea maafa kama tabia hii itaachwa iendelee kuota mizizi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’