Mkufunzi wa magolikipa klabu ya Yanga Milton Nienov ameeleza kufurahishwa na ubora wa magolikipa aliowakutaka katika kikosi jukumu lake sasa likiwa kulinda viwango vyao na kuwaimarisha zaidi
Nienov alitua Yanga mwezi uliopita akichukua nafasi ya Razack Siwa ambaye mkataba wake umemalizika
Kikosi cha Yanga kina magolikipwa wanne Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery, Erick Johora na Godfrey Magaigwa
"Namshukuru Mungu kwa timu yetu kuwa na walinda milango mahiri ambao hawajapishana sana viwango vyao"
"Kazi yetu benchi la ufundi, ni kuboresha viwango vyao , kuvikuza , kulinda na kuweka ushindani ndani yao ili kuleta matokeo chanya kati yao na timu kwa ujumla"
"Tupo katika FA na ligi kuu na malengo ya klabu ni kufanya vyema kwenye ligi zote , hivyo ni lazima kumsaidia kocha mkuu kuandaa wachezaji wote katika ubora mzuri ili awe na uwanja mpana wa kuwatumia"
Kuna majeruhi, majukumu ya timu za Taifa, kadi, matatizo binafsi , kushuka kiwango, n.k, hivyo kama hutakuwa na wachezaji wazuri wenye kuendana viwango kila idara, itakuwa ngumu kushindana na wenzako wenye wigo mpana kwenye uchaguzi wa wachezaji," alisema Milton