Mlinzi wa zamani wa Yanga Ali Mtoni Sonso amefariki dunia leo wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Sonso aliitumikia Yanga msimu wa 2018/19 akitokea Lipuli Fc kisha kusajiliwa na Kagera Sugar mkataba wake ulipomalizika
Msimu huu ameitumikia klabu ya Ruvu Shooting na alicheza mchezo wa mzunguuko wa kwanza dhidi ya Yanga uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-1
Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un
ADVERTISE HERE