Nabi awapa mtihani nyota wapya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Feb 2022
Nabi awapa mtihani nyota wapya

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema ana imani kubwa na vinaja aliowasajili katiak dirisha dogo la usajili

Nabi amesema nyota hao hawapaswi kubweteka baada ya kusajiliwa na Yanga, anahitaji kuwaona wakipambana kuhakikisha wanapata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza

Miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa dirisha dogo ni pamoja na winga Denis Nkane kutoka Biashara United, Chrispine Ngushi kutoka Mbeya Kwanza, Aboutwalib Mshery kutoka Mtibwa Sugar na Ibrahim Bacca kutoka KMKM

Aidha katika dirisha hilo Yanga pia iliwasajiili mkongwe Salum Abubakar kutoka Azam Fc na Chico Ushindi kutoka TP Mazembe

Nabi amesema wachezaji wote wanapaswa kuonyesha ubora wao ili kudhihirisha kuwa benchi la ufundi halikufanya makosa kuwasajili

Aidha akimzungumzia kinda Denis Nkane ambaye alifanya vizuri kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi kule visiwani Zanzibar, Nabi amesema Nkane alipata majeraha lakini hata hivyo amemtaka apambane zaidi

"Napenda kufanya kazi na vijana, unajua vijana wana nguvu, najua Nkane ana maumivu lakini bado sijaridhika na mwanzo wake katika timu, alianza vizuri lakini baada ya kufunga kule Zanzibar kuna aina ya maisha ya kuridhika yamemuingia akilini"

"Hii sio nzuri kwake nimemwambia yeye bado ni mchezaji mchanga asidhani ni staa mkubwa. Yanga imemuamini kuja hapa, anachotakiwa ni kuthibitisha kwamba sisi makocha hatukukosea kumleta hapa. Anatakiwa kupigania namba kwa nguvu na sio kuwa wa kawaida tena," alisema Nabi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’