Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali imeomba mkopo kwa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ili kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kumaliza changamoto zinazolikabili soka la Tanzania
Hivi karibuni AfDB iliridhia kutoa fedha za ujenzi wa barabara za mzunguko Dodoma pamoja na ujenzi wa Uwanja wa Kimataifa wa Msalato
Dk Nchemba alitoa kauli hiyo wakati akimjibu mchambuzi wa soka Shaffih Dauda ambaye kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii aliikosoa klabu ya Yanga kulalamikia mwenendo wa uchezeshaji wa waamuzi ligi kuu ya NBC
Dk Nchemba amesema pamoja na changamoto ya viwanja na waamuzi, kuna shida kubwa hata kwa wachambuzi hivyo wamedhamiria kukomesha UDUMAVU huo

ADVERTISE HERE