Ni suala la muda Ushindi kuanza kikosi cha kwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Feb 2022
Ni suala la muda Ushindi kuanza kikosi cha kwanza

Mashabiki wa Yanga wanatamani kuona winga Chico Ushindi akipewa nafasi ya kuanza kwenye mchezo wa kombe la FA raundi ya tano dhidi ya Biashara United ambao utapigwa Februari 15 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Ushindi ametumika kwa takribani dakika 10 katika kila mchezo dhidi ya Mbuni Fc (kirafiki), Polisi Tanzania, Mbao Fc(FA) na Mbeya City

Katika michezo hiyo Chico alionyesha uwezo mzuri wengi wakifurahishwa zaidi na kiwango alichoonyesha juzi katika mchezo dhidi ya Mbeya City uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana

Chico angeweza kuifungia Yanga bao la ushindi kwenye dakika za majeruhi kama angetumia nafasi ambayo aliitengeneza kwa kushirikiana na Feisal Salum 'Fei Toto'

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema Chico bado hayupo katika utimamu kwa asilimia 100, lakini ameendelea kuimarika

"Chico ni mchezaji mzuri, tulikuwa na sababu ya kumsajili, amejiunga nasi akitoka kwenye majeraha wakati akiitumikia TP Mazembe. Tunaendelea kuimarisha utimamu wake ili awe sawa na wenzake. Nafikiri mashabiki wasiwe na wasiwasi wakati utafika, watafurahia kazi yake," alisema Nabi

Baada ya kulazimishwa suluhu dhidi ya Mbeya City, Yanga inahitaji kushinda mchezo unaofuata wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa Februari 23 uwanja wa Manungu, Morogoro

Yanga inaendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 36, alama tano mbele ya Simba inayoshika nafasi ya pili huku pia Simba waikiwa wamecheza mechi moja zaidi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’