Mlinzi wa Yanga Dickson Job ameomba radhi kufuatia tukio la kumkanyaga kwa bahati mbaya mchezaji wa Mbeya City Richardson Ngondya katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jana
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Job amesema haikuwa dhamira yake kumkanyaga Ng'ondya, kama mchezaji jukumu lake la kwanza ni kulinda afya yake na mchezaji mwenzake
"Mimi kama mchezaji nina wajibu mkubwa wa kulinda afya yangu na ya mchezaji mwenzangu"
"Nimechukua hatua za kuwasiliana na Richardson Ng'ondya na kumjulia hali kutokana na ajali iliyotokea kwenye mchezo wa jana"
"Kamwe sijawahi kuwa na dhamira ya kuhatarisha afya ya mchezaji mwenzangu lakini ajali hutokea mchezoni"
"Nachukua nafasi hii kuomba radhi kwa wote waliosumbuliwa na ajali ile na ahidi kuwa makini zaidi wakati ujao"