Ulikuwa mchezo uliotawaliwa na mbinu - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Feb 2022
Ulikuwa mchezo uliotawaliwa na mbinu - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema walihitaji kushinda mchezo dhidi ya Mbeya City lakini wameyakubali matokeo ya suluhu yaliyopatikana katika mchezo huo

Nabi amesema mchezo ulikuwa wa vipindi viwili ambapo kipindi cha kwanza Mbeya City walikuwa bora katika katika kujilinda wakiweka idadi kubwa ya wachezaji eneo la kati hivyo kuwapa wakati mgumu vijana wake

Nabi amesema mabadiliko ya mbinu aliyofanya kwenye kipindi cha pili yaliongeza kasi ya mashambulizi na kutengeneza nafasi nyingi, lakini hawakuweza kuzitumia

"Ulikuwa mchezo wa kiufundi, Mbeya City walizuia vyema hasa eneo la kiungo uliona kipindi cha kwanza hatukuwa na madhara sana lakini tulibadili mbinu katika kipindi cha pili na tulitengeneza nafasi nyingi lakini hatukuweza kufunga," alisema Nabi

Aidha Nabi ametetea uamuzi wa kutomtumia kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' tangu kipindi cha kwanza akisisitiza kuwa fundi huyo kutoka visiwani Zanzibar hakuwa sababu ya wao kukosa ushindi

"Tatizo halikuwa Feisal, nadhani kama timu tulifanya makosa mengi hasa kwenye kipindi cha kwanza, tulikuwa na nafasi za kufunga mabao lakini hatukuweza kuzitumia. Naheshimu uwezo wa Feisal ni mchezaji mzuri"

Kuingia kwa Feisal kulibadili taswira ya mchezo ambapo Nabi alimtoa David Bryson na kumrudisha Farid Mussa kucheza mlinzi wa kushoto

Feisal amerejea kikosini hivi karibuni baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa wiki mbili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’