Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesisitiza kwa mara nyingine kuwa Yanga bado haijakata tamaa ya kutetea ubingwa wake kwa msimu wa nne mfululizo.
Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting umeifanya Yanga ifikishe alama 25 na kupanda hadi nafasi ya tatu.
Azam FC iko kileleni ikiwa na alama 30 ikifuatiwa na Simba yenye alama 29.
Hata hivyo Simba inaweza kurejea kileleni kama itashinda mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar au hata kutoka sare
Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, Nsajigwa anayeendelea kutekeleza majukumu ya Lwandamina ambaye kibari chake bado hakijapatikana, amesema pamoja na pengo kubwa lililokuwepo kati yao na wanaoongoza ligi bado hawajakata tamaa ya kutetea ubingwa kwasababu bado kuna mechi nyingi sana.
"Hii ligi bado mbichi sana, kuna mechi 16 mbele, hivyo hatuna presha kwani lengo letu liko pale pale kutetea ubingwa wetu."

ADVERTISE HERE